1 3

PRIMARY SCHOOLS/
SHULE ZA MSINGI

Sayansi: Mazoezi ya Kuhitimisha Elimu ya Msingi
J. Nyamwihura & S. Kamugisha
ISBN 9976 973 47 0; 1998; 64pp; Tshs. 2,500.00
Madhumuni ya kitabu hiki ni kuwapatia wanafunzi wa Darasa la Saba mazoezi ya kutosha katika maandalizi ya kufanya mtihani wa kumaliza elimu ya msingi.

 


 

Hisabati za Kikwetu – Majaribio ya Kuhitimisha Elimu ya Msingi - Darasa la nne

 


 

Hisabati za Kikwetu – Majaribio ya Kuhitimisha Elimu ya Msingi - Darasa la Saba
John Nyamwihura & Severin A. Kamugisha
ISBN 9976 973 03 9; 1991; 84pp; Tshs. 2,500.00
Kitabu hiki kimetungwa ili kumpa mwanafunzi mazoezi ya kutosha ya somo la Hisabati tayari kwa mtihani wa Darasa la Saba. Waandishi wanatoa garantii kwamba mwanafunzi atakayepitia maswali yote yaliyo katika kitabu hiki lazima atashinda vizuri somo la Hisabati.

 


 

Mwongozo wa Uelimishaji Rika, Shule za Msingi, Ukimwi na Magonjwa ya Ngono, Darasa la Tano
Yunusi A. Koshuma, Brigitte Jordan-Harder
na Macfydne Sawaya
ISBN 9987 686 25 7; 2002; 28pp; Tshs.2,500.00
Kitabu hiki kinatoa mwongozo wa jinsi ya kubadilishana maarifa katika harakati za kupambana na janga la UKIMWI na magonjwa ya ngono. Kitabu hiki kinatoa mbinu na maarifa ambayo watu katika jumuiya zao wanaweza kujifunza na hivyo kuweza kusaidiana. Ni kitabu cha maana sana katika nyakati zetu. Baadhi ya mada zilizojadiliwa ni pamoja na:

· Ukweli kuhusu VVU/UKIMWI na magonjwa ya ngono;
· Dalili za maambukizo ya VVU na magonjwa ya ngono;
· Kujikinga na VVU na magonjwa ya ngono, na
· Jinsi ya kumhudumia mtu aliyeathirika na UKIMWI.

 


 

Mwongozo wa Uelimishaji Rika, Shule za Msingi, Ukimwi na Magonjwa ya Ngono, Darasa la Sita
Yunusi A. Koshuma, Brigitte Jordan-Harder
na Macfydne Sawaya
ISBN 9987 686 26 5; 2002; 36pp; Tshs.2,500.00
Kitabu hiki kinatoa mwongozo wa jinsi ya kubadilishana maarifa katika harakati za kupambana na janga la UKIMWI na magonjwa ya ngono. Baadhi ya mada zilizojadiliwa katika kitabu hiki ni pamoja na:

· Athari za UKIMWI na magonjwa ya ngono;
· Tabia salama;
· Namna ya kubaki salama katika mazingira hatari; na
· Huduma kwa mgonjwa aliyeathirika kwa UKIMWI.


 

Mwongozo wa Uelimishaji Rika, Shule za Msingi, Ukimwi na Magonjwa ya Ngono, Darasa la Saba
Yunusi A. Koshuma, Brigitte Jordan-Harder, Macfydne Sawaya na Akwillina Mlay
ISBN: 9987 686 26 5; 2002 ; 36pp; Tshs. 2,500.00
Kitabu hiki kinatoa mwongozo wa jinsi ya kubadilishana maarifa katika harakati za kupambana na janga la UKIMWI na magonjwa ya ngono. Baadhi ya mada zilizojadiliwa katika kitabu hiki ni pamoja na:

· Makuzi na mabadiliko wakati wa kubalehe au
kuvunja ungo;
· Afya ya uzazi na ujana;
· Kuepuka imani potofu kuhusu VVU/UKIMWI, mimba na magonjwa ya ngono.
· Matarajio na haki za vijana;
· Unyanyasaji wa kijinsia;
· Ushauri huria na huduma kwa watu wanaoishi na virusi vya UKIMWI; na
· Majukumu ya mwelimishaji, walimu na
kamati za shule.

 


 

Sarufi ya Kiswahili – Shule za Msingi
M. G. Kihampa, B. Mahundi, E. Mwandiko na O. Kagimbo
ISBN 9987-686-56-7 2003 32pp Tshs. 2,200.00
Kitabu hiki kimetayarishwa ili kukidhi mahitaji ya ufundishaji wa sarufi ya Kiswahili katika Shule za Msingi nchini Tanzania. Pia kitawafaa wanafunzi wa Shule za Sekondari na vilevile wageni wanaojifunza lugha hii ya Kiswahili ili waweze kumudu kuiandika na kuizungumza kwa ufasaha.

 

SECONDARY SCHOOLS & COLLEGES/
SHULE ZA SEKONDARI NA VYUO

Uhakiki na Uchambuzi wa Riwaya, Tamthilia na Ushairi Kidato cha Nne
J.P. Mbonde
ISBN 9976 973 58 6; 1999; 67pp; Tshs. 3,000.00
Kitabu hiki kinalenga kumsaidia mwanafunzi kuelewa maudhui ya riwaya, tamthilia na ushairi katika vitabu vya kiada vya fasihi kwa Kidato cha Nne. Hakina lengo la kumfanya mwanafunzi afikiri kuwa anaweza kufaulu mtihani wa fasihi ya Kiswahili bila ya kuvisoma vitabu vyenyewe, na hakikubashiri maswali yatakayotungwa wala kutoa majibu. Kitabu hiki na kile cha Kidato cha Sita vina lengo la kuchochea ari ya wanafunzi kusoma na kuchambua kwa makini, fani na maudhui ya vitabu walivyopangiwa na kuwaonesha maeneo ambayo yatawasaidia kuvielewa vitabu hivyo.

 


 

Uhakiki na Uchambuzi wa Tamthilia, Riwaya na Ushairi, Kidato cha Sita/Vyuo
J.P. Mbonde
ISBN 9976 973 55 2; 2002; 44pp; Tshs. 3,500.00
Kitabu hiki kinalenga kmsaidia mwanafunzi kuelewa maudhui ya tamthilia, riwaya na ushairi katika vitabu vya kiada vya fasihi kwa Kidato cha Sita. Hakina lengo la kumfanya mwanafunzi afikiri kuwa anaweza kufaulu mtihani wa fasihi ya Kiswahili bila ya kuvisoma vitabu vyenyewe; au kama kimejaribu kubashiri maswali yatakayotungwa. Kitabu hiki na kile cha kidato cha Nne vina lengo la kuchochea ari ya wanafunzi kusoma na kuchambua kwa makini, fani na maudhui ya vitabu walivyopangiwa na kuwaonyesha maeneo ambayo yatawasaidia kuvielewa vitabu hivyo.

 


 

Barua Ndefu Kama Hii
Mariama Ba
ISBN 9976 973 21 7; 1994; 128pp; Tshs. 2,500.00
Tafsiri ya riwaya maarufu ya mwandishi huyu wa
Senegal iliyoshinda tuzo ya Noma ya kwanza mwaka 1980. Kiswahili ni lugha ya 18 ilimotafsiriwa riwaya hii. Maudhui makuu ya riwaya hii yamejikita kwenye
harakati za ukombozi wa mwanamke dhidi ya
mfume-dume ulio sugu.

 


 

Vuta N’kuvute
Adam Shafi Adam
9976 973 29 2 1999; Tshs. 5,000.00
Mwandishi aliyekuletea Kasri ya Mwinyi Fuad na Kuli sasa amekuandikia riwaya nyingine, riwaya ya mapenzi inayoanzia Zanzibar na kuishia Tanga, inayounga binti wa Kihindi na kijana wa Kiswahili katika Vuta N’kuvute, ya mapenzi na harakati za siasa za ukombozi.

 


 

Diwani ya Mloka
Charles Mloka
ISBN: 9987 686 44 3 2002 112pp Tshs. 5,000.00
Huu ni mkusanyiko wa mashairi na tenzi mbalimbali zilizoandikwa na Bw. Charles Mloka. Mada za mashairi na tenzi hizi zimejikita kwenye falsafa yake inayogusa nyanja mbalimbali za maisha kama vile: mawaidha na maadili; lugha na fasihi; na siasa na uchumi. Kimo kwenye silabasi ya Darasa la Kumi na Mbili.


 

Elimu Jamii na Chemsha Bongo kwa Mashairi
Charles Mloka
ISBN 9987 686 84 2; 2004; 64pp; TShs. 2,250
Bwana Mloka amejijengea sifa kubwa kama msanii mahili katika fani ya ushairi. Mashairi haya yameandikwa katika sehemu tatu; Elimu Jamii, Siasa na Chemsha Bongo katika lugha fasaha.

 


 

Diwani ya Jinamizi
Ali Salim Zakwany
Mkusanyaji: Abdilatif Abdalla
ISBN: 9987 686 78 8; 2004; 136pp
TShs. 2,500
Kitabu hiki kina tungo za mshairi Ali Salim Zakwany. Tungo zake zimesheheni maarifa na hekima maridhawa kwani zagusa kila nyanja ya maisha ya watu: maadili, elimu, siasa, dini n.k.

 


 

Diwani ya Nyamaume
Khamis Amani Nyamaume; Mkusanyaji: Shaaban C. Gonga;
ISBN: 9987 686 83 4; 2004; 112pp
TShs: 2,500
Kitabu hiki kina tungo za mshairi Khamis Nyamaume wa Dodoma. Tungo zake zafaa kusomwa na kuzingatiwa na watu wa rika zote, kwani zafundisha na kuhekimisha katika mambo mbalimbali ya maisha.

 


 

Guberi Mfawidhi na Ruksa
John Rutayisingwa
ISBN 9987 686 92 6; 2004; 96pp
TShs. 3,000
Riwaya mbili maarufu za marehemu John Rutayisingwa. Ya kwanza inaasa msomaji dhidi ya tabia mbaya katika mahusiano ya wanaume na wanawake. Ya pili inazungumzia matumizi mabaya ya madaraka; lakini katika kula kuna kulipa pia.

 

Education & Textbooks | Children | Art, Literature & Culture | Politics & Economics | Law | Agency Titles | General