
Kanuni na Mbinu za Kufundishia
Toleo la Nne
Mwandishi: S. N. Ndunguru
Kitabu hiki kimeandaliwa ili kuwapa wadau wa elimu na hasa waalimu, nguzo na nyenzo madhubuti katika kupitisha maarifa kutoka kizazi kimoja kwenda kingine. Suala la kukuza ufanisi katika mchakato wa elimu limepewa kipaumbele. Kitabu kimezingatia mbinu za kisasa za ufundishaji ambapo mwanafunzi ndiye mlengwa na mshiriki mkuu katika harakati za kujifunza.
Ni kitabu kitakachowanufaisha wengi, hasa walimu, kwani mwalimu husimama katika ardhi iliyo wakfu kati ya mtoto, jamii na maarifa. Kwa hiyo, ni vyema basi kila mwalimu na kila mzazi ajipatie nakala ya kitabu hiki.
Mwandishi, S. N. Ndunguru, ametumia uzoefu wake wa miaka mingi katika fani ya ualimu ili kuandika kitabu hiki ambacho ni hazina kubwa ya kielimu kwa Watu wa Afrika ya Mashariki na majirani zao. Kwa sasa yeye ni mhadhiri katika Chuo Kikuu Huria cha Tanzania.
Baadhi ya machapisho mengine ya mwandishi ni pamoja na A Wreath for Fr. Mayer, Divine Providence na Spared. |