
Kinyonga mdogo ambaye hakuweza kubadili rangi yake
Mwandishi: Walter Bgoya
Mmoja kati ya watoto thelathini na nane wa Baba na Mama Kinyonga hakuweza kubadili rangi yake kama vinyonga wote wanavyofanya katika kujilinda na nyoka, tai, mwewe na kunguru. Lakini yeye badala ya kujihofia anaahidi kuwalinda wale ndugu zake. Vipi huyu mnyonge ndiyo awe wa kuwalinda wenzake? Soma ugundue kuwa kumbe wale wanaodhaniwa kuwa wadhaifu wanaweza kuwa ndiyo wenye uwezo.
|