Barua Ndefu Kama Hii
Mariama Ba
ISBN 9976 973 21 7; 1994; 128pp; TShs. 2,500.00
Tafsiri ya riwaya maarufu ya mwandishi huyu wa Senegal iliyoshinda tuzo ya Noma ya kwanza mwaka 1980. Kiswahili ni lugha ya 18 ilimotafsiriwa riwaya hii. Maudhui makuu ya riwaya hii yamejikita kwenye
harakati za ukombozi wa mwanamke dhidi ya
mfumo-dume ulio sugu.

 


 

Guberi Mfawidhi na Ruksa
John Rutayisingwa
ISBN 9987 686 92 6; 2004; 96pp
TShs. 3,000
Riwaya mbili maarufu za marehemu John Rutayisingwa. Ya kwanza inaasa msomaji dhidi ya tabia mbaya katika mahusiano ya wanaume na wanawake.
Ya pili inazungumzia matumizi mabaya ya madaraka; lakini katika kula kuna kulipa pia.

 


 

Haramu
James Bwana
ISBN 9987 417 08 6; 2004; 248; TShs. 5,000
Riwaya ya kusikitisha na kusisimua; ya maisha ya Bahati, mtoto ati ‘asiye na baba’, mwenye nuksi.
Katika kutetea utu wake anaua. Soma humu kila aina ya mapambano; ufukara, uonevu, UKIMWI na hatima ingojeayo kugunduliwa.

 

Heri
Zefania J. N. Kalumuna
ISBN: 9987 686 49 4; 2002; 128pp; Tshs. 2,500.00
Hii ni hadithi ya kusisimua ambapo mwandishi wake, ambaye ni mlemavu wa kuona, anaichambua jamii kwa kina na kuweka bayana matatizo mbalimbali na yale yanayotendeka. Kijana Heri anajikuta katika wakati mgumu pale anapobanwa na mambo mbalimbali: mahitaji ya mpenzi wake, Upendo; misukosuko kutoka kwa mama yake wa kambo; misukosuko kutoka kwa walimu wake; misukosuko na adha za usafiri wakati wa kwenda na kutoka shule, na polepole jinsi anavyojitahidi kujikwamua. Baba yake Heri, anampa faraja akimwambia kuwa jina lake, HERI, lina maana kubwa: Hangaikia Elimu Raha Inakungoja. Kisome kitabu hiki ili ufaidi na kuelimika.

 


 

Msako
Mwandishi: Naguib Mahfouz;
Mfasiri: Deogratias M. Simba
ISBN: 9987 686 67 2; 2004; 104pp; TShs: 2,500
Kijana mmoja aliyekuwa akimsaka baba yake ambaye hakuwahi kumfahamu, ananasa katika mapenzi na wanawake wawili na kujikuta kwenye mtego wa mauaji. Je ilikuwaje? Jisomee ugundue visa na mikasa.

 


 

Vuta N’kuvute
Adam Shafi Adam
9976 973 29 2 1999; Tshs. 5,000.00
Mwandishi aliyekuletea Kasri ya Mwinyi Fuad na Kuli sasa amekuandikia riwaya nyingine, riwaya ya mapenzi inayoanzia Zanzibar na kuishia Tanga, inayounga binti wa Kihindi na kijana wa Kiswahili katika Vuta N’kuvute, ya mapenzi na harakati za siasa za ukombozi.