Diwani ya Jinamizi
Ali Salim Zakwany
Mkusanyaji: Abdilatif Abdalla
ISBN: 9987 686 78 8; 2004; 136pp
TShs. 2,500
Kitabu hiki kina tungo za mshairi Ali Salim Zakwany. Tungo zake zimesheheni maarifa na hekima maridhawa kwani zagusa kila nyanja ya maisha ya watu: maadili, elimu, siasa, dini n.k.

 


 

Diwani ya Mloka
Charles Mloka
ISBN: 9987 686 44 3 2002 112pp Tshs. 5,000.00
Huu ni mkusanyiko wa mashairi na tenzi mbalimbali zilizoandikwa na Bw. Charles Mloka. Mada za mashairi na tenzi hizi zimejikita kwenye falsafa yake inayogusa nyanja mbalimbali za maisha kama vile: mawaidha na maadili; lugha na fasihi; na siasa na uchumi. Kimo kwenye silabasi ya Darasa la Kumi na Mbili.

 


 

Diwani ya Nyamaume
Khamis Amani Nyamaume;
Mkusanyaji: Shaaban C. Gonga;
ISBN: 9987 686 83 4; 2004; 112pp
TShs: 2,500
Kitabu hiki kina tungo za mshairi Khamis Nyamaume wa Dodoma. Tungo zake zafaa kusomwa na kuzingatiwa na watu wa rika zote, kwani zafundisha na kuhekimisha katika mambo mbalimbali ya maisha.

 


 

Elimu Jamii na Chemsha Bongo kwa Mashairi
Charles Mloka
ISBN 9987 686 84 2; 2004; 64pp; TShs. 2,250
Bwana Mloka amejijengea sifa kubwa kama msanii mahili katika fani ya ushairi. Mashairi haya yameandikwa katika sehemu tatu; Elimu Jamii, Siasa na Chemsha Bongo katika lugha fasaha.

 


 

Maisha ya Mchagga Hapa Duniani na Ahera
Petro Itosi Marealle
ISBN 9976 973 91 8; 2002; 166pp; Tshs. 6,000.00
Kitabu hiki kinahusu masuala mbalimbali ya kabila la Wachagga wa Kilimanjaro: mila, desturi, historia na imani yao katika mambo ya Mungu na mengineyo, hususan mwingilio wa wageni na tamaduni zao. Ni kitabu kinachotoa mafundisho mengi si kwa watu wa kabila hilo tu bali kwa watu wa makabila yote na wote wanaotetea na kulinda mila na desturi za makabila yao. Ni kitabu kitakachowaelimisha wengi: walimu, wanafunzi, wanahistoria, wana-elimu-jamii na wengine, katika nyanja za historia, utamaduni na maendeleo ya wanadamu kwa ujumla. Kitawasaidia pia watu wa makabila mengine kuhifadhi katika maandishi mila, desturi, historia na tamaduni zao.

Fasihi ya Shaaban Robert

Kielezo cha Fasili
Shaaban Robert
ISBN: 9976 973 15 2 1991 112pp Tshs. 3,000.00
Fasili ni maelezo ya fikira na maono katika karaa, aghalabu ya mashairi. Ni taaluma katika maandiko ya lugha na fahamu ya fikira za mwandishi kwa msomaji, ni msaada katika ustadi wa fasaha na wa tungo. Tunawakaribisha Watanzania, hasa vijana, kukisoma, kuburudishwa na kufunzwa na yale aliyoyaandika kwa sanaa na kipaji adimu cha mshairi wa taifa marehemu Shaaban Robert.

 


 

Kufikirika
Shaaban Robert
ISBN: 9976 973 06 3; 1991; 68pp Tshs. 2,250.00
Kufikirika ni nchi moja kubwa katika nchi za dunia. Kaskazini imepakana na Nchi ya Anasa, Kusini Nchi ya Majaribu, Mashariki Bahari ya Kufaulu na Magharibi Safu ya Milima ya Jitihadi. Ramani ya nchi hiyo ni adimu kupatikana kwa sababu nchi yenyewe haiandikiki ila hufikirika kwa mawazo tu. Njia ya kwenda nchi hiyo hukanyagwa kwa fikira siyo nyayo. Endelea kusoma hadithi hii yenye hekima nyingi na misingi ya falsafa.

 


 

Kusadikika
Shaaban Robert
ISBN: 9976 973 10 1; 1991; 80pp; Tsh. 2,500
Kusadikika ni nchi ambayo kuwako kwake hufikirika kwa mawazo tu. Nchi hiyo iko katikati ya mipaka sita. Kwa kuvichapisha tena vitabu vya marehemu Shaaban Robert, tunarejesha fasihi ya Tanzania katika kiwango chake kileleni ili rika ya sasa ielewe utajiri wa taifa katika fani ya ushairi.

 


 

Maisha Yangu na Baada ya Miaka Hamsini
Shaaban Robert
ISBN: 9976 973 16 0 1991 136pp Tshs. 3,250.00
Hiki ni kitabu cha marehemu Shaaban Robert juu ya maisha yake mwenyewe. Ni kitabu cha kusisimua. Kinatoa picha halisi ya mwandishi huyu maarufu katika Afrika ya Mashariki. Mwandishi huyu ameacha urithi mkubwa wa hekima katika nyanja mbalimbali za maisha ya mwanadamu na kuna mengi ya kuvutia na hata kusikitisha katika maisha yake nyakati za enzi za ukoloni hapa nchini.

 


 

Mapenzi Bora
Shaaban Robert
ISBN: 9976 973 08 X; 1991; 80pp Tshs. 2,500.00
Mapenzi ni jambo muhimu sana katika maisha ya binadamu. Lakini mapenzi yapi? Shaaban Robert anaeleza kwa ufasaha na sanaa, Mapenzi Bora. Kimo kwenye silabasi ya Darasa la Kumi na Nne.

 


 

Wasifu wa Siti Binti Saad
Shaaban Robert
ISBN 9976 973 09 8; 1991 88pp Tshs. 2,500.00
Kitabu hiki ni moja ya wasifu bora kabisa zilizowahi kuandikwa juu ya binadamu. Mwandishi wetu maarufu, Shaaban Robert, ametuachia kumbukumbu muhimu sana juu ya mwanasanaa na mwanaharakati wa aina yake, yaani Siti Binti Saad. Kwa kusoma wasifu huu, tunaona mambo mbalimbali, mojawapo ni utetezi wa haki za wanawake na wanyonge, ukombozi wao dhidi ya ugandamizaji wa kila aina na kadhalika. Kimo kwenye silabasi ya Darasa la Kumi na Nne.