Hotuba ya Kufungua Mdahalo wa Kitaifa
Juu ya Maendeleo

Benjamin W. Mkapa
Mwaka wa Uchapishaji: 2004
ISBN: 9987 686 77 X; 2004; 32pp; TShs. 1,500
Katika kitabu hiki, Rais Benjamin Mkapa anazungumzia masuala kadhaa na hatua za serikali katika kuleta maendeleo ya Watanzania pamoja na changamoto ambazo hawana budi kukabiliana nazo ikiwa
wanataka maendeleo.

 


 

Kazi za Taasisi ya Mwalimu Nyerere
Baba wa Taifa, Mwalimu J.K. Nyerere
ISBN 9987 686 80 X; 2001; 44pp; TShs: 1,750
Mwalimu alieleza kazi za Taasisi yenye jina lake katika Bunge na kutoa maelezo fasaha ya masuala muhimu aliyotaka Taasisi hiyo ijishughulishe nayo. Wale wanaotaka kuielewa Taasisi hiyo wataelimishwa na kijitabu hiki.

 


 

Misingi Bora ya Uandaaji wa Miradi
L. J. Mshana
ISBN 9987 686 84 2; 2004; 64pp; TShs: 2,000
Maandalizi ya miradi mbalimbali ni hatua muhimu katika mchakato wa maendeleo. Kitabu hiki kitawawezesha walimu na wanafunzi kupata stadi za kushiriki ipasavyo katika sekta ya umma.

 

Uwazi na Ukweli: Rais wa Watu Azungumza na Wananchi. Kitabu cha Kwanza
Benjamin William Mkapa
ISBN 9987 686 43 5 2003 pp Tshs 4,000.00
Kitabu hiki ni cha kwanza katika mfululizo wa hotuba za Rais wa Awamu ya Tatu wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania anazotoa kila mwisho wa mwezi. Upekee katika hotuba hizi ni kwamba mada zake mbalimbali ambazo zinagusa masuala yanayohusu maendeleo ya nchi ya Tanzania na watu wake zinatolewa na kiongozi mkuu katika utungaji na utekelezaji wa sera. Ni kitabu muhimu cha rejea kwa wanafunzi wa Shule za Sekondari, Vyuo vya Elimu na Vyuo Vikuu, wafanyabiashara, wanasiasa, wanaharakati wa maendeleo ya binadamu, wakulima na wananchi wote katika kuimarisha uraia bora na uelewa wa masuala ya siasa, uchumi na jamii.

 


 

Uwazi na Ukweli: Rais wa Watu Azungumza na Wananchi. Kitabu cha Pili
Benjamin W. Mkapa
ISBN 9987 686 76 1; 2004; 212pp; TShs: 4,500
Kitabu cha Pili cha hotuba za kila mwisho za mwezi za Rais Mkapa, mwaka 2002. Hotuba hizi ni ufunguo wa uelewa sahihi wa siasa, uchumi na masuala ya jamii yetu katika kipindi hiki cha historia.

 


 

Uwazi na Ukweli: Rais wa Watu Azungumza na Wananchi. Kitabu cha Tatu
Benjamin W. Mkapa