2 3

Ali Baba na majangili arobaini
Hassan Adam
Vielelezo: Abdul Gugu
ISBN 9987 686 91 5; 2004; 50pp; TShs. 3000
Hadithi hii ni ya mkata kuni fukara aliyegundua na kuokota dhahabu iliyofichwa kutoka pangoni na majangili arobaini. Hadithi hii maarufu ni moja katika hadithi za Uajemi na Uarabuni ziitwazo alfu lela u lela, imesimuliwa na Bairu Katama.

 


 

Asiyesikia la Mkuu Huvunjika Guu
Mariam Abdi
Vielelezo: Cloudy Chatanda
ISBN 9987 686 96 6 2004 24pp Tshs. 2000.00
Kijana Jabir anakosa usikivu kwa wazazi wake. Anajiingiza katika mambo yasiyofaa. Siku moja anakutana na tukio moja linalombadilisha. Ni tukio gani hilo? Fuatilia.

 


 

Fisi na Kucha za Simba
Marco Mussa
Vielelezo: Godfrey Semwaiko
ISBN 9987-686-22-2 2002 24pp Tshs. 2,000.00
Fisi hakujua kwamba ukiona vyaelea ujue vimeundwa. Aliazima kucha za Simba yakampata yaliyomtoa kanga manyoya. Je, ni yapi hayo? Fualitia kisa hiki upate uhondo.


 

Hadithi ya Kunguru na Chura Mzee
Walter Bgoya
Vielelezo: Christine Steinberg-Mund
ISBN: 9987 686 42 7 2002 20pp Tshs. 3,000.00
Kunguru mwenye nguvu anashindwa katika mbio na chura mwendapole. Kumbe wenye nguvu hawashindi kila mara na wadogo nao wanastahili kusikilizwa. Hadithi yenye mafunzo ya busara.

 


 

Hadithi ya Kunguru na Kaa
Walter Bgoya
Vielelezo: Christine Steinberg
ISBN: 9987417205
TShs. 3,000
Kaa anaelekea ufukoni akitafuta chakula. Mara Kunguru wawili wanataka kumla. Nani atashinda? Ili ufahamu mwisho wake soma kitabu hiki chenye kufurahisha.

 


 

Hadithi Isiyo na Mwisho
Abdu Haji Mjaka
Vielelezo: Godfrey Semwaiko
ISBN: 9987 686 14 1 2002 24pp
Tshs. 2,200.00
Mfalme Tayari ni mpenda hadithi sana. Pia binti yake aitwaye Hafidha anapenda sana hadithi kama baba yake. Siku moja binti akamwambia baba yake kuwa angependa aolewe na mwanamume atakayeweza kumsimulia hadithi isiyo na mwisho. Mfalme akawatangazia vijana wanaume wajaribu bahati yao. Je, atapatikana msimulizi wa hadithi isiyo na mwisho na kumwoa binti mfalme?

 


 

Hasira Hasara
Hassan Adam
Vielelezo: Cloudy Chatanda
ISBN 9987 417 07 8; 2004; 40pp; TShs. 3,000
Mkusanyiko wa hadithi nyingi za wanyama zenye maadiii

 


 

Hadithi ya Katope Mtoto Aliyeumbwa kwa
udongo mwekundu

Walter Bgoya
Vielelezo: Abdul Gugu
ISBN 9987 417 13 2; 2004; 30pp; TShs: 3000
Katope ameumbwa na wazee wawili mke na mume ambao hawakuwa na watoto, ktokana na udongo mwekundu. Lakini ni lazima Katope asinyeshewe na mvua. Soma uone ni namna gani aliepuka mvua na nini kilimpata alipojikuta akiwa amechelewa kuiepa.

 


 

Hadithi ya Morile
Freda Mariki
Vielelezo: Abdul Gugu
ISBN 9987 417 06 X; 2004; 24pp; TShs. 2,000
Hadithi ya mapokeo ya kabila la Wachagga. Inasimulia jinsi kijana Morile alivyojipatia kitoto kutokana na kiazi. Baadaye alivyokosana na wazazi wake na hatimaye kupaa juu ambako alijipatia utajiri mkubwa kutokana na maarifa yake ya moto. Je, alirudi vipi duniani? Wazazi wake walimpokeaje? Soma upate kufahamu.

Jini na Mayai ya Ajabu
Mehta Abeid
Vielelezo: Prof. Francis Msangi
ISBN 9976 973 27 6 1999 14pp Tshs. 1,000.00
Selenge na Muza walikuwa marafiki wakubwa. Walikuwa wakienda porini na kusaka sufi kwa ajili ya kutengeneza magodoro na mito. Siku moja Selenge alikwenda porini peke yake akatokewa na Jini ambaye kutokana na utii wa Selenge, alimpa mayai ya ajabu ambayo yalimtimizia shida zake zote. Muza kwa kuona wivu naye alikwenda porini ili apewe mayai kama hayo. Soma kitabu hiki ili upate kujua ni nini kilichotokea baada ya Muza kupewa mayai na kushindwa kutimiza masharti ya yule jini.

 


 

Katala na Genge la Wezi
Jackson Kalindimya
Vielelezo: Cloudy Chatanda
ISBN 9987 686 90 7; 2004; 24pp; TShs. 2,000
Katala ni mpenzi mkubwa wa mpira. Anacheza mpira
kila mahali. Katika harakati za mchezo huo, anapiga shuti kubwa ambalo linaingia mpaka jikoni na kuvunja vyombo. Mchezo unaishia hapo. Anapopewa mpira, inakuwa ni baada ya siku nyingi.
Safari hii yeye na rafiki zake wanakwenda kucheza
mbali zaidi. Mpira unasaidia kugundua maficho ya genge la wezi. Ni kwa namna gani, fuatilia.

 


 

Kinyonga Mdogo Ambaye Hakuweza Kubadili Rangi Yake
Walter Bgoya
Vielelezo: Christine Steinberg-Mund
ISBN: 9987 686 53 2 2003 20pp Tshs. 3,000.00
Mmoja kati ya watoto thelathini na nane wa Baba na Mama Kinyonga hawezi kubadili rangi yake kama vinyonga wote wanavyofanya katika kujilinda na nyoka, tai, mwewe na kunguru. Lakini yeye badala ya kujihofia anaahidi kuwalinda wale ndugu zake. Vipi huyu mnyonge awe ndiye wa kuwalinda wenzake? Soma ugundue kuwa kumbe wale wanaodhaniwa kuwa wadhaifu wanaweza kuwa ndio wenye uwezo.

 


 

Kisa cha Binti Mfalme na Mpiga Zeze
Mehta Abeid
Vielelezo: Abdallah Gugu
ISBN 9976 973 26 8; 1994; 40pp; Tshs. 1,000.00
Bahati ni bahati na ushujaa ni ushujaa. Mara chache vinaambatana. Mpiga zeze fukara anatumia zeze lake na ushujaa kumpata binti mfalme kuwa mkewe.

 


 

Kaona Njigi Kadhani Njege
Laurent Kamugisha
Vielelezo: Godfrey Semwaiko
ISBN 9987 686 17 6; 2002; 24pp; Tshs. 2,000.00
Msichana mrembo aliyeitwa Tigaina alimwona mwanamke mwenye ushanga ambao ulimvutia sana.
Ni ushanga kama huo uliomfanya aone njigi akidhani njege. Je, nini kilimpata? Fuatilia uone msemo huu una maana gani.

 


 

Kisa cha Ng’ombe na Simba
Abdi Mkindi
Vielelezo: Abdul Gugu
ISBN 9987 686 87 7; 2004 24pp Tshs. 2,000.00
Kukosana katika maisha ni jambo la kawaida. Kusameheana huleta maelewano zaidi na kuleta maisha. Kutosamehe huleta mauti na maumivu.
Mwana Simba hakuwa tayari kusamehe, hatimaye alipatwa na maumivu.

 


 

Kuku Mweusi na Kenge
Sauda S. Kilumanga
Vielelezo: Abdul Gugu
ISBN 9987 686 92 3 2004 32pp Tshs. 2,500.00
Kuku anataga mayai yake.Kumbe kuna mwizi mjanja aibae na kula mayai yale. Kenge. Lakini siku za mwizi ni arobaini na kwa kila ujanja kuna ujanja unaoushinda. Kuku anamlisha jiwe Kenge badala ya yai. Soma ugundue alifanyaje na mwisho wake.

 


 

Lango la Ajabu
Deogratias M. Simba
ISBN 9976 973 98 5; 2002 ; Tshs. 2,000.00
Maisha yamejaa mfululizo wa mapambano.
Maendeleo yanakuja kwa kukabiliana vyema na changamoto mbalimbali tunazopata katika maisha. Kijana Sankuta anakabiliana na changamoto ngumu kwa ujasiri mkubwa na akili nyingi ambayo, hatimaye, inamfikisha katika kilele cha mafanikio, ufalme. Hii ni hadithi inayokusudia kuwashajiisha vijana kukabiliana vyema na changamoto za maisha. Licha ya hilo, pia inaburudisha na kuchangamsha. Ni hadithi ambayo kila kijana hana budi kuisoma.