1 3

Majivuno Yamuua Samaki
Peter Dominic
Vielelezo: Peter Dominic
ISBN 9987 686 98 2; 2004; Tshs. 2,500.00
Kweli majivuno ni kitu kibaya. Katika hadithi hii tamu, samaki anapoteza maisha yake kwa sababu ya kutaka sifa. Picha nyingi za rangi zinavutia sana na zitawapa raha watoto.

 


 

Masimulizi ya Alfu Lela U Lela, Kitabu cha 1
Mfasiri: Hassan Adam
220 ISBN 9987 417 02 7; 2004; 220pp
TShs. 6,000
Kitabu hiki kina hadithi maarufu duniani kote zenye asili ya Arabuni na Uajemi. Tafsiri za awali simulizi hizi hazikuwa kamilifu, kwa maana ya kwamba, baadhi ya masimulizi hayakujitokeza, hivyo kuwakosesha watu uhondo kamili. Hii ndiyo tafsiri ya kwanza kamili ya hadithi hizi.

 


 

Masimulizi ya Alfu Lela U Lela, Kitabu cha 2
Mfasiri: Hassan Adam
ISBN 9987 417 03 5, 2004; 194pp; TShs. 5,500
Hiki ni kitabu cha pili katika mfululizo wa hadithi nyingi na maarufu duniani kote za Alfu Lela U Lela zenye asili ya Arabuni na Uajemi.

 


 

Maringo ya Kinyonga
Elizabeth Mwandiko
Vielelezo: Peter Dominic
ISBN 9987 686 85 0; 2004; 24pp; Tshs. 2,500.00
Katika mashindano ya michezo, ishirikishayo wanyama na ndege, amini usiamini, Kinyonga anaibuka mshindi. Picha nzuri za rangi zitawavutia watoto wa umri huu.

 


 

Nataka Kuwa Tajiri
Opportuna J. Mosha
Vielelezo: Cloudy Chatanda
ISBN: 9987 417 01 9; 43pp; TShs. 1,750
Masumbuko alitaka kupata utajiri kwa haraka, akatoroka shule kwenda mjini na akaishia mahabusu. Alipata matatizo mengi na kujifunza. Fuatilia kisa hiki kwa makini ili ujifunze na kuelimika.

 


 

Nora na Matunda ya Ajabu
Mary G. Kihampa na Deogratias M. Simba
Vielelezo: Godfrey Semwaiko
ISBN 9987 686 184; 2002; 24pp; Tshs. 2,000.00
Nora ni mtoto mtiifu na mwenye adabu. Sifa nyingine aliyonayo ni udadisi na kutaka kujielimisha zaidi. Ni katika udadisi wake huu ambapo anakutana na matunda ya ajabu aliyotumwa kwenda kuyanunua sokoni. Je, ni maajabu gani hayo? Fuatia kisa hiki upate kufahamu.

Nyani Mtu
Rashid Mohamed Zahor
ISBN 9987 686 93 1; 2004; 24pp; TShs. 2,500
Nyani anabadilika kuwa mwanamke mzuri anaolewa na binadamu na kuzaa watoto. Lakini baadae anaanza kuota manyoya, mkia, kubadilika sura na kurudia asili yake ya nyani. Kwani ilikuaje? Jisomee ugundue

 


 

Popo, Ndege na Panya
Hamisi Akida
Vielelezo: Godfrey Semwaiko
ISBN: 9987-686-40-0 2002 20pp Tshs. 2,200.00
Popo alikuwa akirandaranda na kuzurura akitafuta
familia ambayo ingeweza kumpokea na kumpenda. Kwanza alikwenda kwa panya lakini panya walimkana. Halafu alikwenda kwa binadamu, na huyo ndiye kabisa akamtimua. Baadaye akaenda kwa ndege, hao pia walimkataa. Lakini mambo yalikuja kugeuka. Waliomkataa wakataka sasa awe jamaa yao.
Soma ugundue hawa ni akina nani na nini kilitokea.

 


 

Saa Ngapi?
Sauda S. Kilumanga
Vielelezo: Abdul Gugu
ISBN: 9987 686 94 X 2004 36pp Tshs. 2,500.00
Kuku anataga mayai yake.Kumbe kuna mwizi mjanja aibae na kula mayai yale. Kenge. Lakini siku za mwizi ni arobaini na kwa kila ujanja kuna ujanja unaoushinda. Kuku anamlisha jiwe Kenge badala ya yai.
Soma ugundue alifanyaje na mwisho wake.

 


 

Safari Kwenye Nchi ya Maajabu
Fatma S. Rawah
Vielelezo: Abdul Gugu
ISBN: 9987 686 95 8; 2004; 28pp;
Tshs. 2,500.00
Samira mtoto mtukutu, mvivu hapendi kusoma wala kufanya kazi. Usiku mmoja anaota ndoto ya kutisha. Anabebwa na dege moja kubwa hajui wapi.
Soma ugundue anapelekwa wapi na anarejea kwa masharti gani?

 


 

Safari ya Kuvumbua Mwisho wa Dunia
Deogratias M. Simba
Vielelezo: Abdul Gugu
ISBN 9987 417 12 4; 2004; 40pp; TShs. 2,500
Vijana wawili wanaamua kwenda kuutafuta mwisho wa dunia. Wanashindwa katika jaribio lao la kwanza. Baadaye wanasafiri kwenda Dar es Salaam.
Huko wanajifunza mengi, ikiwa ni pamoja na njia saba za kuthibitisha kwamba dunia ni duara. Je, njia hizo ni zipi? Fuatana na Sankuta na Kassessabunga katika safari yao hii ya ajabu.