
Ua la Zalizali
Mehta Abeid
Vielelezo: Godfrey Semwaiko
ISBN 9987 686 19 2 Cp 2002 32pp Tshs. 2500.00
Hali ya ulemavu au nyingineyo isiyo ya kawaida katika mwili wa binadamu si sababu ya kutosha ya kumfanya mhusika kushindwa kujiletea maendeleo na kujipatia mafanikio maishani. Katika hadithi hii ya kusisimua, kijana Deli anafaulu kushinda hali ya ugonjwa alionao mwilini mwake na hatimaye kuweza kujipatia mafanikio makubwa ambayo mwanadamu yeyote angependa ayapate. Je, alitumia siri na mbinu gani? Soma unufaike.
 Uadui wa Kunguru na Nyoka
Peter Dominic
Vielelezo: Peter Dominic
ISBN 9987 686 99 0 2004 20pp TShs. 2,500/=
Nyoka anamkabidhi Kunguru mayai yake ayalinde. Kunguru anayala. Nyoka nae anayala makinda ya Kunguru. Yalianzaje hayo na yaniashia wapi? Jisomee ugundue Uadui wa Kunguru na Nyoka.

Ushujaa wa Fatuma
Fedha S. Bosse
Vielelezo: Abdul Gugu
ISBN 9987 686 89 3 Cp 2004 48pp Tshs. 2500.00
Ni heka heka za sherehe ya harusi. Watu wazima wanakimbia na kuhangaikia shughuli hiyo. Wanatoa nafasi ndogo kwa watoto. Hawawasikilizi. Hawawajali. Msichana shujaa, Fatuma, anatumia mbinu ya hali ya juu kuwakumbusha watu wazima kuwa hata wao, yaani watoto, wapo pia. Alifanyaje, soma.

Watoto na Zimwi
Fidelis Beya
Vielelezo: Godfrey Semwaiko
ISBN 9987 686 206 2002 20pp Tshs. 2000.00
Vijana wawili, Soli na Demi, wanapambana na zimwi Mla Watu. Zimwi huyu pamoja na wenzake walishambulia watu pamoja na mifugo yao. Mashujaa wengi waliteketea katika kutetea jamii ya wanadamu. Ni Soli na Demi ambao hatimaye walifaulu kummaliza Zimwi Mla Watu. Je, walitumia ujanja gani? Walipata nini baada ya hapo? Fuatilia kisa chenyewe upate majibu ya maswali haya.
|
|

Wimbo wa Bata Bukini
Hassan Adam
Vielelezo: Cloudy Chatanda
ISBN 9987 417 06 X; 2004; 28pp; TShs. 3,000
Mkusanyiko wa hadithi nyingi za wanyama zenye adili.

Wimbo wa Nyenje
Hamisi Akida (mfasiri)
ISBN 9976 973 22 5; 1994; 20pp; Tshs. 1,500.00
Nyenje alikuwa hodari wa kuimba na alipendwa sana na wenzake ila Meya ambaye alimwonea wivu. Meya naye alitaka kuwa mwanamuziki lakini sauti yake ilikuwa mbaya na hakuweza kushindana naye. Siku moja viumbe wale waliingiliwa na adui. Licha ya wingi wao viumbe wale hawakuweza kumwondoa yule adui mpaka walipomkumbuka Nyenje aliyekuwa gerezani.
Jisomee ujue Nyenje aliwasaidiaje kumshinda adui na yale yaliyompata Meya.

Zimwi la Mrima
Fatma S. Rawah
Vielelezo: Abdul Gugu
ISBN: 9987 417 05 1; 2004; 20pp; TShs. 2,500
Hadithi hii inamhusu kijana Mayuga aliyechukuliwa kama punguani. Lakini ujasiri na ubunifu wake unamwezesha kuuwa zimwi na kukomboa wasichana liliowateka. Mfalme anamwoza binti yake na sasa Mayuga anakuwa mtu mkubwa.
|